Ukubwa na Udogo

Maneno huwekwa katika ukubwa au udogo yanapozidi kiasi cha wastani kinachotarajiwa. Hali ya ukubwa na udogo hutumika hasa unaposifia au kudharau kitu.

Ukubwa

Nomino zote katika hali ya ukubwa huwa katika ngeli ya LI-YA. Tunaweka maneno katika ukubwa kwa kuongeza kiungo JI na/au kutoa kiwakilishi cha ngeli.

Udogo

Maneno huwekwa katika udogo ili kusifia udogo wao au kudharau kiasi chake. Nomino zote katika hali ya udogo huwa katika ngeli ya KI-VI. Maneno huwekwa katika udogo kwa kuongeza kiungo ki- au kiji-. Katika baadhi ya maneno, kiambishi kiwakilishi cha ngeli huachwa nje tunapoweka maneno katika udogo.

Wastani

Hii ni hali ya kawaida/katikati ya nomino. Si kubwa si ndogo.

WASTANI UDOGO UKUBWA
1. mtu kijitu jitu
2. mto kijito jito
3. kitu kijikitu jikitu
4. mtoto kitoto / kijitoto toto / jitoto
5. mlango kijilango lango
6. mwiko kijimwiko / kijiko jimwiko
7. chungu kijichungu jungu
8. nyumba chumba / kijumba jumba
9. kikapu kijikapu kapu / jikapu
10. mji kijiji jiji