Ngano za Mazimwi
Hizi ni ngano ambazo baadhi ya wahusika wake ni majitu makubwa yenye uwezo ukiamaumbile (uliozidi wa kawaida). Mazimwi ni viumbe waliobuniwa na binadamu ambao wanaweza changanya sifa zi binadamu, za mnyama na za shetani. Aghalabu mazimwi hufanya maovu kama vile kula watu.
Sifa za Mazimwi
- Mazimwi yanaweza kuwa na mchanganyo wa sifa za kibinadamu, za wanyama na za kishetani.
- Mazimwi huwa na maumbile yasiyokuwa ya kawaida kama vile pembe, mikono mitatu, jicho la nyuma n.k
- Mazimwi yana uwezo wa kujibadilisha kutoka umbo moja hadi jingine. k.v mti, msichana, kisima, nyoka n.k
- Mazimwi huwa adui kwa wanadamu na huwaangaisha sana kwa kuwala, kuwatisha, kuwaibia, kuwaharibia mali na kuvuruga amani katika jamii.
- Wanaohangaishwa sana na mazimwi ni wanawake, watoto na watu wanaotembea usiku au kwenda katika maeneo fulani.
- Aghalabu zimwi hushindwa nguvu na kufa. Kwa mara nyingi, watu walioliwa/kumezwa na jitu hutokeza kabla ya kifo chake.
- Aghalabu, hadithi za mazimwi huwa na mwisho maalum, k.v tangu siku hiyo waliishi raha mustarehe.
Umuhimu wa Ngano za Mazimwi
- Kutahadharisha watu wawe makini.
- Kutuonya dhidi ya maovu kama vile ulafi, tamaa n.k
- Kuhimiza utiifu
- Kuburudisha
- Kupitisha muda