Kisengere Nyuma na Kisengere Mbele

Kisengere Nyuma (Flashback)

Pia huitwa Mbinu Rejeshi. Mwandishi 'hurudi nyuma' na kuanza kusimulia kisa kilichokuwa kimetendeka kabla ya alichokuwa akisimulia. Aidha, mwandishi hubadilisha wakati wa masimulizi na kuwa wakati wa kisa hicho. Hutumika sana kuonyesha mhusika anapokumbuka kitu, au kutupatia msingi wa jinsi mambo yalivyoanza

  • Mhusika Y wanakutana na Mhusika Z. Kisha kila mmoja anamtambua mwenzake. Wanaanza kukumbuka maisha yao ya utotoni, namna walivyojuana. Kila mmoja anakumbuka kana kwamba mambo hayo yanafanyika wakati huu.
  • Aria na Hanna wako katika kituo cha polisi. Wanaonekana na wasiwasi mwingi sana. Masaa matatu kabla ya hayo, Aria anamkuta Hanna amesimama kando ya mwili wa Alison. 'Nini kinaendelea?' Aria anamwuliza Hanna. 'Sijui, nilijikuta hapa.' 'Labda mtu alikupatia dawa na kukuleta hapa ili uonekana kama ulimwuua Alison. Tutoke hapa!' Wanaanza kuondoka, lakini polisi wanawashika. Sasa wawili hao wameketi hapo kwa hofu, kwani hawana uhakika kwamba polisi wataawamini. Ofisa mmoja anawaita ndani.

Kisengere Nbele (Foreshadow)

Mwandishi anapobadilisha wakati na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni; au kutumia lugha isiyo moja kwa moja kutabiri yatakayojiri.

  • Baada ya Sara na Saidi kukumbatiana, Sara anaanza kutafakari jinsi maisha yatakavyokuwa. Wanatazama runinga na Saidi na watoto wao watatu. Watoto wanaenda kulala. Wanabaki sebuleni wakizungumzia habari za siku hiyo. Wanabusiana na kwenda kulala. Hiyo itafanyika tu, iwapo Saidi atamwuliza wachumbiane.
  • Latifa anamtesa sana Kesha. Laiti angalijua kwamba dunia ni duara. Siku yake ya arubaini iko njiani yaja.