Kuchanganya Ndimi

Kuchanganya Ndimi

Kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili.
  • Nimempigia minister huyo simu na amekubali kunipatia hiyo contract kuanzia next month .
  • Kasuku hapatikani home kila kunapo wedding ceremony katika kijiji hiki.

Kuhamisha Ndimi

Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu.
  • Ikiwa hataki kukubali, acha kubishana naye. Afterall, if you argue with a fool we might not know the difference. Mwache tu.