Mafumbo

Mafumbo ni aina ya tungo fupi ambazo huwa na maelezo yanayoishia kwa swali; kisha anayejibu huhitajika kufikiria ili kutambua jibu. Kinyume na vitendawili, majibu ya mafumbo huwa na maelezo marefu.

Sifa za Mafumbo


  1. Mafumbo huwa na sehemu mbili – sehemu ya swali na sehemu ya jibu.
  2. Huwa baina ya watu wawili – anayefumba na anayefumbua (wanaofumbua)
  3. Mafumbo yaliendelezwa wakati maalum.
  4. Jibu la fumbo si maalum kwani kinachohitajika ni mantiki katika jibu.

Umuhimu wa methali


  1. Hukuza uwezo wa kufikiri ili kupata jibu.
  2. Huimarisha umoja katika jamii kwani watu huja pamoja wanapofumbiana mafumbo.
  3. Mafumbo huhifadhi utamaduni – hupokezanwa kutoka kizazi hadi kizazi
  4. Mafumbo hutumika kama burudani
  5. Hutumika kupitisha muda.

Mifano ya mafumbo


  1. Fumbo: Ajali mbaya ilitokea kati ya mpaka wa Kenya na Tanzania. Je, majeruhi walizikwa wapi?
    Jibu: majeruhi hawakuzikwa, walikimbizwa hospitalini
  2. Fumbo: Upepo ulikuwa unavuma sana kutoka mashariki hadi magharibi. Nilikuwa nikiliendesha gari la moshi linalotumia umeme kutoka Burundi hadi Malawi. Je, moshi ulielekea upande gani?
    Jibu:Gari la moshi linalotumia umeme halitoi moshi
  3. Fumbo: Mimi na ndugu yangu tulinunua fahali mmoja kutoka sokoni. Baada ya mwaka mmoja alijifungua ndama wawili. Je kila mtu alipata wangapi?
    Jibu: ndama hajifungui
  4. Fumbo: Juma ana vitu vitatu; mbwa, kuku na mchele anaotaka kuvusha mto. Mbwa hula kuku na kuku hula mchele. Kulingana na sheria za kuvuka daraja lile, hauwezi kuvuka ukiwa na zaidi ya vitu viwili. Je juma atatumia njia gani kuvuka?
    Jibu: kwanza atavusha mbwa na mchele kisha atarudi na kumchukua kuku.