Malumbano ya Utani

Malumbano ya utani ni mashindano ya kuongea jukwaani baina ya watu wa makundi au jamii mbili ambayo hutumia kejeli na chuku kukejeli tabia mbaya katika jamii au kundi fulani. Watu husimama jukwaani na kushindana kwa maneno.

Sifa za Malumbano ya Utani


  1. Hutumia mzaha na vichekesho
  2. Hutumia kinaya na kejeli ili kuangazia ukweli fulani katika jamii

Umuhimu wa Malumbano ya Utani


  1. Kurekebisha mambo mabaya katika jamii
  2. Kuburudisha
  3. Kupitisha muda