Maonyesho ya Sanaa

Maonyesho huhusisha watu wa jamii au kundi fulani wanaoonyesha taaluma, ujuzi au sanaa yao kwa watazamaji. Kwa mfano maonyesho ya kilimo, maonyesho ya kitamaduni n.k Mazingira katika maonyesho haya huwa ni maeneo halisi na wahusika wake huwa watu halisi katika familia.

Mifano ya Sanaa ya Maonyesho

a) Maonyesho ya Kilimo


Katika maonyesho haya, wakulima kutoka sehemu mbalimbali huonyesha bidhaa zao za kilimo kama vile vyakula, mifugo, mbegu na kadhalika. Nia ya maonyesho ya kilimo huwa ni kuwaelimisha watu kuhusu mbinu bora za ukulima.

b) Maonyesho ya Kisayansi


Haya ni maonyesho ya mbinu mpya za kisayansi na teknolojia.

c) Maonyesho ya Kitamaduni


Jamii mbalimbali huonyesha utamaduni wao mbele ya hadhira kama vile nyimbo za kitamaduni na sherehe nyingine

d) Maonyesho ya Kibiashara


Katika maonyesho ya kibiashara, bidhaa mpya huonyeshwa kwa hadhira. Kampuni mbalimbali hujitokeza kufahamisha hadhira kuhusu bidhaa zao mpya.

Sifa za Sanaa ya Maonyesho


  1. Huwa na matangazo kusifia bidhaa, mbinu au mawasilisho mbalimbali
  2. Aghalabu huwa na mashindano ambayo washiriki hushinda zawadi mbalimbali
  3. Wahusika huwa watu halisi katika jamii
  4. Hutumia mazingira halisi badala ya kutumia jukwaa

Umuhimu wa Sanaa ya Maonyesho


  1. Kufahamisha watu kuhusu bidhaa na mbinu mpya
  2. Kuburudisha
  3. Kuleta watu pamoja