Miviga
Miviga ni sherehe mbalimbali katika jamii fulani. Watu hujumukika na sherehe hizi kulingana na tamaduni zao. Watu mbalimbali katika jamii huwa na majukumu tofauti tofauti. Miviga huandamana na nyimbo, vyakula na mawaidha kutoka kwa wazee. Mifano ya miviga ni kama vile Sherehe za ndoa, mazishi, tohara n.k
Sifa za Miviga
- Huandamana na nyimbo zinazohusiana na sherehe hiyo kwa mfano nyimbo za mazishi, ndoa n.k
- Ngoma mbalimbali huchezwa
- Huwa na vyakula vya kienyeji
- Aghalabu kina mama hupewa kazi za upishi na burudani
- Wazee hutoa mafunzo, mawaidha kwa vijana
Umuhimu wa Miviga
- Huleta jamii pamoja na kuunganisha watu katika jamii
- Watu hupata mafunzo kutoka kwa wazee katika jamii
- Hudumisha tamaduni katika jamii
- Huburudisha - kwa mfano sherehe zinapohusisha nyimbo na michezo ya kuigiza
- Huliwaza - kwa mfano wakati wakati wa huzuni kama vile mazishi