Mnyambuliko wa Vitenzi

Mnyambuliko wa vitenzi ni jinsi vitenzi vinavyobadilika kulingana na kauli/hali mbalimbali. Kwa mfano kutokana na kitenzi 'soma' tunawezapata somea, somewa, somwa n.k. Ni vizuri kuelewa kwamba sio vitenzi vyote vinavyonyambulika katika kila kauli.

Kwa sasa tutaangalia kauli zifuatazo. Ili kukusaidia uelewe kauli hizi vizuri, tutakutumia wewe kama mfano na mtu mwengine; lakini mnyambuliko unaweza kutumika kwa kitu chochote kila. :

Mifano Katika Jedwali

TENDA TENDEA TENDANA TENDEANA TENDWA TENDEWA TENDEKA TENDESHA TENDESHANA
fanya fanyia fanyana fanyiana fanywa fanyiwa fanyika fanyisha fanyishana
Lima Limia Limana Limiana Limwa Limiwa Limika Limisha Limishana
Pika Pikia Pikana Pikiana Pikwa Pikiwa Pikika Pikisha Pikishana
Lia Lilia ? Liliana ? Liliwa Lilika Liza Lizana
kula lia lana liana liwa liwa lika lisha Lishana
penda pendea pendana pendeana pendwa pendewa pendeka pendeza pendezana
omba ombea ombana ombeana ombwa ombewa ombeka ombeza ombezana
tembea tembelea tembeleana tembeleana tembelewa tembelewa tembeleka tembeza tembezana
abudu abudia abudiana abudiana abudiwa abudiwa abudika abudisha abudishana

Hivi karibuni tutakuletea mnyambuliko katika kauli za kutendua, kutendeshea, kutendesheana, kutendata, kutendama n.k. Isitoshe tutakuletea mnyuambuliko wa vitenzi vya silabi moja.