Ngomezi

NGOMEZI
Pia Huitwa Sanaa ya Ngoma
Utanzu wa Fasihi Fasihi Simulizi
Kipera cha Maigizo

Prev Miviga
Next Malumbano ya Utani

Ngomezi ni sanaa ya ngoma. Midundo tofauti tofauti ya ngoma hutumika kuwakilisha ujumbe au maana fulani. Ngoma zilitumika sana kabla ya teknolojia ya barua na simu. Wataalam wa ngoma walipiga ngoma kwa milio mbalimbali kufahamisha jamii kwa jambo fulani limefanyika kwa mfano kuingia kwa adui, moto, mtoto anapozaliwa n.k

Sifa za Ngomezi


  1. Hutumia midundo mbalimbali ya ngoma kupitisha ujumbe fulani
  2. Huhitaji mtaalam wa ngoma
  3. Maana ya midundo mbalimbali hubadilika kutoka kwa jamii moja hadi nyingine, hivyo basi ni vigumu kwa jamii-adui kutambua ujumbe wake

Umuhimu wa Ngomezi


  1. Kupitisha ujumbe
  2. Kutahadharisha jamii dhidi ya adui
  3. Kuburudisha
  4. Kuhifadhi tamaduni za jamii


  • Comments