Soga (Mazungumzo)

Soga ni mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi ambayo aghalabu huwa hayana mada maalum. Aghalabu soga huwa na vichekesho vingi, mzaha na kejeli. Nia yake huwa kuburudisha na kupitisha wakati.

Sifa za Soga


  1. Soga huwa na vichekesho na mzaha mwingi
  2. Mada hubadilikabadilika kutoka wakati mmoja hadi mwingine
  3. Haihitaji taaluma yoyote ya kisanaa
  4. Inaweza kufanyika mahali popote - njiani, sebuleni, katika vyumba vya burudani n.k

Umuhimu wa Soga


  1. Kupitisha wakati hasa watu wanaposubiri jambo fulani lifanyike kama vile chakula kiive
  2. Kuburudisha
  3. Kuunganisha jamii