Taashira

Ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika hali fulani yenye uhusiano na kile kilichotumiwa. Vitu vinayotumika katika taashira ni vitu vinavyofahamika na watu wengi kwa ujumla kuwa na uhusiano na hali inayowakilishwa.

Ifuataya ni mifano ya baadhi ya vitu ambavyo hutumiwa kuwakilisha dhana / hali nyingine.
  • Maji - kuwakilisha uhai
  • Wekundu - kuwakilisha hatari, damu, mapenzi
  • Nuru - tumaini, hekima, wazi
  • Giza - ukosefu wa hekima, ukosefu wa tumaini, dhambi, siri

Mifano ya Taashira

  • Mama Tumaini alipouawa, giza lilitanda. Watoto wake hawakujua la kufanya.
  • Mwanamke Msamaria alipewa maji ya kunywa na Bwana Yesu
  • Mganga Kuzimu huvalia nguo nyeusi nyeusi