Takriri

Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Isitoshe, takriri inaweza kujitokeza kwa kurudia rudio wazo fulani katika kazi ya sanaa. Repetition .
  • Tumechoshwa na siasa mbaya. Tumechoshwa na ahadi zisizotimizwa. Tumechoshwa na miradi isiyo kamilika. Tumechoshwa na malumbano na migogoro ya kikabila. Tumechoka.
  • Hongera hongera Bwana Kisaka, hongera kwa ujasiri wako. Hongera! uliyoyatenda ni raha kwetu. hongera