Tashbihi

Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha; 'kama', 'mithili ya', 'sawa na', 'ja'. Pia huitwa tashibiha, tashbiha . Similes
  • mweusi kama makaa
  • mweupe kama theluji
  • mrembo mithili ya malaika
  • baridi kama barafu
  • pumbafu kama kondoo
  • mwembamba kama sindano
  • maridadi kama kipepeo
  • mtundu kama tumbili
  • pendana kama chanda na pete
  • adimika mithili ya maziwa ya kuku