Tashihisi

Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu). Pia huitwa uhuishaji . Personification .
  • picha hii imekuwa ikinikodolea macho tangu asubuhi
  • Fikira zangu zilikuwa zikizunguka kwenye ajali niliyoshuhudia siku hiyo
  • Upepo mkali umeyafukuza mawingu yakatoweka angani na sasa jua linatuwanga kwa hasira.