Upeo

UPEO WA JUU / UPEO WA CHINI
Kitengo Tamathali za Usemi
Aina ya Mbinu za Sanaa
KIINGEREZA
Upeo wa Juu Climax
Upeo wa Chini Anti-climax

Prev Njozi
Next Mbinu ya Nyimbo

Upeo wa Juu (climax)

Ni sehemu ya hadithi ambayo matukio yanafanyika kulingana na mapenzi ya hadhira au msomaji.

  • Siri tuliyokuwa tukiisubiri kwa hamu na ghamu imefumbuliwa. Tunashusha pumzi.
  • Ingawa walipitia dhuluma chungu nzima, wahusika wakuu tunaowaopenda, wanawashinda maadaui zao; wanaoana na kuishi kwa raha mustarehe.

Upeo wa Chini (anti-climax)

Ni sehemu ya hadithi ambayo matukio yanafanyika kinyume na mapenzi ya hadhira au msomaji. Aghalabu upeo wa chini hutokea baada ya upeo wa juu.

  • Baada ya vifungu vilivyojaa vituko kemkem, mambo yanatulia; tushafumbuliwa mafumbo yote lakini bado hadithi inaendelea.
  • Siku chache baada ya mhusika mkuu kuibuka mshindi, anavamiwa na kuuawa. Anazikwa kwa huzuni nyingi sana.


  • Comments