Vichekesho

Vichekesho ni aina ya sanaa ya fasihi simulizi ambayo watu hutoa vihadithi vifupi au sentensi zenye uwezo wa kuwafanya wasikilizaji wacheke. Vichekesho huhitaji ubunifu mwingi ili kutaja jambo litakalowavunja bavu hadhira.

Sifa za Vichekesho


  1. Huwa na uwezo wa kutekenya hisia hadi mtu acheke.
  2. Aghalabu vichekesho huwa vifupi
  3. Hutumia mifano ya vitu vinavyojulikana wazi na hadhira katika mazingira/mandhari yao.
  4. Hutumia mbinu ya kejeli na chuku sana.

Umuhimu wa Vichekesho


  1. Kuburudisha
  2. Kupitisha wakati