Vitanza Ndimi na Vichezea Maneno
Vitanza Ndimi na Vichezea Maneno ni vipera vya Tungo Fupi katika Fasihi Simulizi
Vitanza Ndimi
Vitanza Ndimi (tongue twisters) huwa ni sentensi zinazotumia maneno yanayomkanganya msomaji katika matamshi. Vitanza ndimi huhitaji kutamkwa haraka haraka na kurudiwa rudiwa mara kadhaa kwa kusudi la kukuza uwezo wa kutamka.
k.m:
- Shirika la reli la Rwanda lilishirikiana na shirika la reli la Libya.
- Ni zipi zikusikitishazo?
Vichezea Maneno
Vichezea Maneno (word play) maneno yanayokaribiana kimatamshi au kimaana hutumika katika sentensi moja kama njia ya kuonyesha ukwasi wa lugha au kuburudisha. Pia hutumika kama vitanza ndimi.
- Nitasisitiza na nitasita kusitasita.
- Kanga wa Mahanga mwenya matanga anatangatanga Tanga