Istiara

Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo 'ni' ama 'kuwa'. Pia huitwa sitiari, stiari

Tofauti kuu kati ya Istiara na jazanda ni kwamba isitiara hulinganisha kwa kutumia kiungo "ni" au "kuwa" ilhali jazanda haitumii kiungo chochote.

Kwa mfano:
  • Isitiara: - Atoli ni kobe, atakuchelewesha njiani.
  • Jazanda: - Ukitemembea na kobe yule, atakuchelewesha njiani.

Mifano ya Istiara

  • Mwalimu wetu ni simba, usifanye kosa lolote.
  • Bwana ni jabali langu.
  • Mama wa kambo amekuwa mamba, nyumbani hamkaliki
  • Anita ndiye nuru katika familia yao.
  • Masomo nayo yamekuwa mawe.