Khurafa
Kwa kuwa wahusika wote katika hadithi za aina hii ni wanyama kutoka mwanzo hadi mwisho, hatuwezi kusema kwamba mbinu ya uhuishaji/tashihisi imetumika.
Sifa za Khurafa
- Wahusika wake ni wanyama wenye uwezo wa kuongea na kufanya kama binadamu
- Hurejelea maswala yanayopatikana katika jamii zetu kama utendaji kazi, ukuzaji uchumi, uongozi, utangamano katika jamii, n.k
- Funzo lake huwa wazi kv tamaa, ujinga n.k
Umuhimu wa Khurafa
- Kuburudisha hadhira
- Kuelimisha watoto kuhusu wanyama mbalimbali na sifa zao
- Kukuza maadili katika jamii
- Kuelekeza na kunasihi
- Kupitisha muda
Mifano
MNYAMA | SIFA |
Sungura | tabia za ujanja - sungura huwakilisha watu wasiopenda kuchoka/kufanya kazi lakini hutumia ujanja wao kula jasho la wengine, au kuwaangamiza adui zao. |
Simba | kwa mara nyingi simba hutumika kama kiongozi/mfalme - huwakilisha watu wenye ukali katika jamii, ambao wakiongea husikika na huogopewa sana. |
Fisi | Ni mhusika mwenye tamaa na ulafi ambaye fikira zake zimetawaliwa na tamaa yake. Fisi hutumika kuwakilisha wanadamu wazembe na wajinga, wasiopenda kufikiria sana kwani mawazo yao yamejikita katika tamaa zao. |
Nyani | Anapotumika katika hadithi, hudhihirisha hekima na uwezo wa kufanya uamuzi wa busara. Nyani hutumika sana kama hakimu na huwakilisha viongozi wenye hekima katika jamii. |
Nyoka | ni mnyama mwenye hila na huwakilisha watu wenye hila katika jamii. |
Kobe | huwakilisha watu wanyamavu, ambao japo wanajua kufanya kitu, hawapendi kuchangia, lakini mwisho huibuka washindi; watu wasiokimbilia kufanya mambo |
Ndovu | huwakilisha watu wenye kimbelembele, ambao hujisifu na kujitafutia umaarufu. Watu wa aina hii hupenda kuwa katika msitari wa mbele japo huenda hawana ujuzi wa kutosha katika jambo lilo. |