Lakabu
Lakabu ni majina yanayobandikwa watu kutokana na sifa zao, maumbile, hulka au mambo yanayowahusu.
Kama vile semi, lakabu ni tungo fupi ambazo zinaweza kutumika kama Mbinu za Lugha na Sanaa
Tofauti kuu kati ya lakabu na majazi ni kwamba majazi ni jina halisi la mtu ilhali lakabu ni jina la kupachikwa.
Mifano ya Lakabu
- Katika riwaya ya Siku Njema , mhusika mkuu (Msanifu Kombo) hubandikwa jina la "Kongowea Mswahili" kwa kufanya bidii sana na kubombea katika lugha ya Kiswahili.
- Mama Rita anapenda kuongea sana. Hivyo basi wanakijiji wakambandika jina, Kasuku.