Maswali ya Balagha

Maswali ya balagha ni maswali ambayo msimulizi au mhusika hujiuliza bila kulatarajia jibu. Umuhimu wa maswali haya ni kuchochea fikira za hadhira. Pia huitwa mubalagha, tashititi, tashtiti . Rhetorical Questions . Maswali haya yanaweza kujitokeza katika uzungumzi nafsia ambapo mhusika hujiongelesha kana kwamba anazungumza na mtu mwengine.