Mighani au Visakale
Sifa za Mighani
- Hutumia chuku kusifia matendo na uwezo wa shujaa.
- Majagina huwa na uwezo wa ukiamaumbile (uwezo unaozidi wa binadamu)
- Huwa ni vigumu sana kwa shujaa kuuawa minghairi ya idadi ya maadui wake
- Shujaa huwa na siri kuu ya nguvu zake (kama nguvu kuwa kwenye kivuli, nywele, n.k)
- Jagina hupigania haki za jamii yake
- Jamii ya jagina huwakilisha wema ilhali maadui wao huwakilisha ubaya.
- Jagina hufa mwishoni, haswa baada ya kusalitiwa na mtu wake.
- Hadithi hizi huaminika kuwa za kweli ama zenye kiwango fulani cha ukweli; kwamba mashujaa hao walikuwa.
Sifa za Jagina (Shujaa)
- Huwa na nguvu zinazotokana na siri fulani
- Wana uwezo wa ukiamaumbile
- Hupigania haki za jamii yao
- Huwa na kimo kisichokuwa cha kawaida k.v mfupi sana, mrefu sana n.k
- Aghalabu huwa watu wema kulingana na maadili ya jamii zao.
Umuhimu wa Visakale
- Kuunganisha jamii
- Kuhifadhi historia ya jamii
- Kuelimisha, kunasihi na kuelekeza
- Kuburudisha
- Kupitisha muda
Mifano ya Majagina
JAGINA | KABILA | |
Mekatilili wa Menza | Giriama | Mwanamke aliyeongoza wanandi dhidi ya wakoloni |
Fumo wa Linyongo | Wapate | Vita dhidi ya Sultani wa Pate |
Kinjeketile Ngwale | Wamatumbi | Majimaji Rebellion |
Luanda Magere | Luo | Vita dhidi ya Wanandi |
Koitalel arap Samoei | Nandi | Nandi Rebellion |
Shaka | Zulu | Aliongezea ufalme wa Kizulu |