Semi - Misemo na Nahau
Semi ni mafungu ya maneno yanayotumiwa kuleta maana nyingine badala ya maana halisi ya maneno yaliyotumika.
Kwa mfano tukisema mtu amegonga mwamba hatumaanishi kwamba amepiga jiwe kubwa kwa mkono au kwa kifaa chochote, bali tunamaanisha kwamba ameshindwa kuendelea katika jambo fulani.
Semi ni kipera cha tungo fupi katika fasihi simulizi; na hutumiwa katika aina nyingine za sanaa kama tamathali za lugha. Kuna fani mbili za Semi:
Umuhimu wa Semi
- Kupunguza ukali wa maneno k.m: amega dunia badala ya amekufa
- Kupamba lugha
- Kuhifadhi mali amali ya lugha/jamii
Mifano ya Nahau
NAHAU | MAANA |
Kupiga moyo konde | kujituliza/kujiliwaza |
Kujipa moyo | kujiliwaza |
Kupiga hatua | kuendelea mbele |
Kukata kamba | kuaga dunia |
Kupiga darubini | kufanya uchunguzi |
Kutupa macho | kuangalia mbali |
Kupigwa kalamu | kufutwa kazi |
Kuandaa meza | kutayarisha chakula |
Kugonga mwamba | kutofanikiwa |
Kwenda msalani | kwenda chooni |
Mifano ya Misemo
MSEMO | MAANA |
Mkono wa birika | uchoyo |
uzi na shindano | ushirikiano |
Shingo upande | bila kupenda |
kiguu na njia | mtu asiyetulia mahali pamoja |
Mdomo na pua | karibu sana |
Lila na fila | mema na mabaya |