Ngano za Usuli (Visaviini)

Ngano za usuli husimulia asili au chanzo cha dhana fulani. Visasili hukusudia kuelezea kwa nini jambo fulani hutokea au kwa nini vitu huwa kama vilivyo. Kwa mfano kwa nini fisi huchechemea, kwa nini kobe hutembea polepole n.k. Hujibu swali: Kwa nini jambo fulani huwa jinsi lilivyo?

Tanbihi: Tofauti kati ya visasili na usuli(visaviini) ni kwamba visasili huhusisha jamii fulani, mila, imani na matukio ya kiada kama vile kifo, tohara n.k ilhali ngano za usuli huelezea kwa nini mambo fulani hufanyika bila kuhusisha jamii au imani.

Sifa za Usuli


  1. Hueleza aili ya dhana/hali fulani ulimwenguni.
  2. Huwa na mwanzo maalum - kuonyesha kwamba katika zama za kale dhana inayorejelewa, haikuwa vile ilivyo sasa.
    Mfano:
    1. Hapo zamani za kale, kobe alikuwa na ngozi laini kama wanyama wengine...
  3. Huwa na mwisho maalum - kuthibitisha kwamba yaliyosimuliwa katika hadithi hiyo ndiyo yaliyopelekea kuwepo kwa hali hiyo.
    k.m:
    1. ...Hii ndiyo sababu ngozi ya kobe ina magamba.
    2. ... Tangu siku hiyo fisi huchechemea.
    3. ... na hadi wa leo kuku hutazama juu anapokunywa maji.

  4. Hurejelea dhana zinazopatikana katika ulimwengu wa sasa.


Umuhimu wa Usuli

  1. Kuelimisha watoto kuhusu mazingira na dhana mbalimbali
  2. Kutafuta maelezo ya mambo yanayochukuliwa kuwa ya kawaida.
  3. Kuelekeza na kunasihi
  4. Kuburudisha hadhira
  5. Kukuza uwezo wa kufikiri
  6. Kupitisha muda



Mifano

  1. Kwa nini fisi huchechemea
  2. Kwa nini ngozi ya Kobe ina magamba
  3. Kwa nini chura ana mabaka katika ngozi yake
  4. Kwa nini kanga hana manyoya
  5. Kwa nini Paka na panya ni maadui