Visasili (Visa-asili)
Tanbihi: Tofauti kati ya visasili na usuli(visaviini) ni kwamba visasili huhusisha jamii fulani, mila, imani na matukio ya kiada kama vile kifo, tohara n.k ilhali ngano za usuli huelezea kwa nini mambo fulani hufanyika bila kuhusisha jamii au imani.
Sifa za Visasili
- Huelezea chimbuko la jamii fulani
- Matokeo yake hufanyika mwanzoni (k.v mwanzo wa dunia)
- Aghalabu huhusisha miungu, malaika n.k
- Kuburudisha
Umuhimu wa Visasili
- Kutafuta jibu kwa maswali yanayotatiza
- Kuhifadhi historia na imani ya jamii
- Kuunganisha jamii
- Kuwasilisha mila na desturi za jamii
Mifano
- Asili ya jamii ya Wamaasai
- Asili ya Wagikuyu